Home » Viongozi Wa Kike Baringo Wataka Serikali Kuingilia Kati Kukomesha Pombe Haramu

Viongozi Wa Kike Baringo Wataka Serikali Kuingilia Kati Kukomesha Pombe Haramu

Biashara haramu ya pombe katika lokesheni ya Sabatia kaunti ndogo ya Koibatek, imeendelea kuwa na athari kubwa kwa maisha ya vijana,huku viongozi wa akina mama wakijitokeza na kudai hatua kuchukuliwa kukomesha biashara hizo.

Katika kijiji cha Kabyemit iliyoko kwenye kata ndogo ya Solian, viongozi wa akina mama wanadokeza kwamba biashara ya pombe inazidi kuwa na athari kubwa katika maisha ya jamii, na hasa vijana ambao ndio tegemeo la siku za baadaye.

https://mideyahdigital.co.ke/2023/01/13/holy-dave-afikishwa-mahakamani/

Akizungumza kwa niaba ya akina mama katika hafla moja ya hadhara kwenye kata ya Solian, Mary Taalam alisema vilabu vya pombe vinazidi kupata umaarufu kwani pia zinatenga maeneo ya kuwafuruhisha watoto wachanga ili kutoa fursa kwa wazazi kushiriki unywaji mbele ya watoto wao.

Katika maeneo mengi ya Baringo ikiwemo tarafa ya Mochongoi iliyoko kwenye eneobunge la Baringo Kusini, wananchi wamezidi kuendesha mikutano za kujadili athari za pombe kwa maisha ya binadamu.

https://mideyahdigital.co.ke/2023/01/13/celebrating-a-life-well-lived/

Katika juhudi za kupunguza idadi ya vilabu mashinani, serikali ya Baringo inaombwa kutupilia mbali utegemeaji wa ushuru kutoka kwa pombe  kwa madai kwamba,biashara  hiyo ya pombe inasababisha hasara kubwa kwa kizazi cha binadamu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!