Home » Wahudumu Wa Magari Wataka Serikali Kupunguza Bei ya Mafuta Kufikia Kesho Saa Sita

Wahudumu Wa Magari Wataka Serikali Kupunguza Bei ya Mafuta Kufikia Kesho Saa Sita

Madereva na wahudumu wa magari wameitaka serikali kupunguza bei ya mafuta kuanzia kesho saa sita.

Wakiongozwa na Geofrey Mwaniki, madereva hao wamesema uchumi umezidi kupanda na bei ya sasa ya mafuta inakuwa ngumu kwao kuimudu.

Wakati huo huo naye John Kamau amesema wamiliki wa magari ya umma wanakosa faida kutokana na bei ya juu ya petroli na ubovu wa barabara ambao unawafanya kutengeneza magari yao kila kukicha.

Serikali kupitia mamlaka ya EPRA hutangaza bei za mafuta kila mwezi tarehe 14 ambazo huanza kutekelezwa siku inayofuata hadi tarehe 14 ya mwezi unaofuata.

Katika bei ambayo itaacha kutumika kesho, petroli Nakuru inauzwa kwa shilingi 176.62, Diseli shilingi 161.83 kwa lita, na mafuta taa shilingi 45.79 kwa lita moja.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!