Home » Sipendi Waafrika Nataka Kuolewa na Mzungu, Huddah Monroe Asema

Sipendi Waafrika Nataka Kuolewa na Mzungu, Huddah Monroe Asema

Picha kwa hisani

Mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe amesema kamwe hatokuja kuolewa na Mwafrika kwa sababu ataendelea kuteseka na umaskini.

Huddah alisema kuwa kama kuna mwanaume ambaye atakubali kumtolea posa bila kupepesa, ni Mrusi.

Kwa mujibu wa Huddah, bara zima la Afrika halina musitakabali angavu na kutwa kucha ni kuhangaika na umaskini, jambo ambalo hakuumbiwa yeye.

“Mustakabali wa Afrika si angavu hata kidogo asikudanganye mtu. Nataka mwanamme wa Urusi haraka iwezekanavyo. Siwezi olewa na Mwafrika kwa sababu tutaendelea kujigaragaza katika mateso yale yale ya bara la Afrika,” Huddah aliandika.

Huddah ambaye kwa muda mrefu amekuwa akionesha chuki yake kwa nchi yake Kenya na Waafrika wote hadharani aliwahi nukuliwa akisema kuwa yeye hutumia muda mwingi nje ya nchi kama vile Dubai katika kile alisema kuwa Kenya hakuna sehemu nzuri za kujivinjari na huwa hajihisi salama akiwa Kenya.

https://mideyahdigital.co.ke/2023/01/12/shambulizi-la-kigaidi-yafeli-diani-uchunguzi-waanzishwa/

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!