Home » Holy Dave Afikishwa Mahakamani!

Msanii wa injili nchini Kenya Holy Dave amefikishwa katika mahakama ya Kibera kwa madai ya kumpiga kichwani mfanyabiashara moja kwa kutumia chupa ya pombe katika klabu ya usiku huko Kilimani, Nairobi.

Holy Dave ambaye aliachiwa kwa dhamana , alikana mashtaka ya kumshambulia Keem Daudi na kumsababishia majeraha mabaya mwilini.

Hata hivyo, wapelelezi wa kesi hiyo wamefanikiwa kuzipata picha za CCTV ambazo zitatumika kama ushahidi katika kesi hiyo.

https://mideyahdigital.co.ke/2023/01/13/mwili-wa-mtoto-wa-darasa-la-sita-wapatikana-ndani-ya-gunia-loitoktok/

Mahakama ilifahamishwa kuwa mnamo Oktoba 1, mwaka 2022, Holy Dave alimshambulia mwathiriwa baada ya kuingia kwenye ugomvi alipokuwa akimtetea rafiki yake ambaye alitaka kujiunga naye katika sehemu ya watu mashuhuru klabuni hapo lakini alikuwa akizuiwa na walinzi

https://mideyahdigital.co.ke/2023/01/13/celebrating-a-life-well-lived/

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!