Mwili Wa Mtoto Wa Darasa La Sita Wapatikana Ndani Ya Gunia Loitoktok

Taharuki imetanda katika kijiji cha Maili Tisa, Loitoktok kaunti ya Kajiado baada ya wanakijiji kupata mwili wa mtoto wa darasa la sita umekatwa katwa na kufungwa ndani ya gunia.
Msichana huyo wa Darasa la Sita aliripotiwa kutoweka Januari 4 na wazazi wake na hivyo kusababisha msako mkali.
Inasemekana kuwa macho ya msichana huyo yalinyofolewa, mguu wake wa kulia ulikatwa na kuchunwa ngozi.
Kamanda wa Polisi wa Kajiado Kusini, Shadrack Ruto anasema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa msichana huyo pia alinajisiwa.
Mwili huo ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya kaunti ndogo ya Loitokitok ukisubiri kufanyiwa upasuaji.