Home » Shambulizi La Kigaidi Lafeli Diani!

Maafisa wa upelelezi mjini Mombasa wanataka muda zaidi wa kuwachunguza watu watatu wanaohusishwa na shambulizi la kigaidi lililofeli katika mkesha wa mwaka mpya katika klabu kimoja huko Diani kaunti ya Kwale.

Musab Abdulnasir Kassim, Mistwah Abdulnasir Kassim, na Aisha Abdalla Musa walifikishwa katika mahakama ya Mombasa jana lakini hawakushtakiwa.

Badala yake, afisa wa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi (ATPU) Japheth Yagan, amewasilisha hati nyingine ya kiapo akiomba muda zaidi wa kuwachunguza watatu hao, akidai kuwa siku saba alizopewa wiki jana hazikutosha kukamilisha uchunguzi.

Imefichuka pia kuwa bastola ya Glock yenye muundo wa Austria iliyopatikana kutoka kwa washukiwa hao iliyokuwa na risasi 15 ilitumika kutekeleza uhalifu mkubwa katika eneo la Kisauni, Kaunti ya Mombasa.

Mpelelezi huyo pia amefichua kuwa bunduki iyo hiyo ingetumika kutekeleza uhalifu Mombasa wakati wa msimu wa likizo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!