Home » Maisha jela kwa Mwanaume Aliyenajisi na Kumuoa Mtoto wa Miaka 10

Maisha jela kwa Mwanaume Aliyenajisi na Kumuoa Mtoto wa Miaka 10

Saigulu Ololosereka,50, mwanaume anayutuhumiwa kunajisi na kuoa mtoto wa miaka 10 Picha kwa hisani

Mahakama ya Narok imemhukumu mwanamme mwenye umri wa miaka hamsini kifungo cha maisha jela, baada ya kukiri kosa la kunajisi na kuoa msichana wa miaka kumi.

Saigulu Ololo-sereka, ambaye alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Narok, Phyllis Shinyanda, alishtakiwa kwa makosa mawili: kumnajisi msichana wa miaka kumi na kumuoa mtoto huyo kinyume na sheria mwaka wa 2019.

Shinyanda alieleza katika uamuzi wake kuwa mwanamme huyo alionywa juu ya uzito wa kesi hiyo baada ya kukiri shtaka hilo, lakini akashikilia kuwa alimuoa msichana huyo kwa sababu wazazi wa binti huyo walimtoa kwake kwa ajili ya ndoa.

Shinyanda aliendelea kusema kuwa uhalifu huo ulikuwa mkubwa na wa kinyama, na kwamba mwathiriwa alilazimika kuvumilia miaka mitatu ya kutendewa unyama.

Hakimu Mwandamizi aliendelea kusema kuwa kitendo hicho cha kinyama kilikuwa na athari za muda mrefu za kisaikolojia na kimwili kwa sababu msichana huyo alikeketwa kabla ya kuolewa na baadaye kufanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua.

Mtuhumiwa ana siku 14 za kukata rufaa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!