Madalali Wafurushwe Marigat!

Wafugaji katika eneo la Marigat wanataka serikali ya Baringo kuharakisha mpango wa kugeuza mfumo wa kuuza mifugo katika kaunti hiyo, ili kuondoa madalali wanaowanyanyasa wakulima wa ngombe, mbuzi na kondoo.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima wa eneo bunge la Baringo Kusini, Robert Milalo ambaye ni mfugaji anasema uuzaji wa mifugo kwa kutumia macho inasababisha hasara kwa mkulima, kwani madalali hutumia fursa hiyo kuwanyanyasa wakulima.
Mkulima huyo anatoa wito huu wakati ambapo shule zinakaribia kufunguliwa kwa muhula wa kwanza mwezi huu huku wazazi wakisaka karo.