Msanii Jackie Chandiru Aumbua Vituo Vya Rehab!

Msanii wa Uganda Jacky Chandiru Eyaa.
Hitmaker wa “Gold Digger”, Msanii Jackie Chandiru amedai kwamba kituo cha matibabu cha watumizi wa dawa, pombe na mihadarati hakikuwahi kumsaidia kujiepusha na uraibu wa dawa za kulevya.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema hamkatishi tamaa mtu yeyote anayetamani kwenda Rehab ila kwa upande wake hali yake ya kiafya ilidorora zaidi alipokuwa chini ya uangalizi wa kituo hicho.
Chandiru ametoa kauli hiyo alipoulizwa kutoa maoni yake kama King Saha atanufaika na uangalizi wa kituo cha matibabu cha watumiaji wa dawa za kulevya
Itakumbukwa mapema wiki iliyopitwa msanii King Saha alikimbizwa hospitali baada ya kuugua ugonjwa unaodaiwa kusababishwa na uraibu wake wa kutumia mihadarati.
Lakini habari njema kwa mashabiki ni kwamba madaktari walimruhusu kwenda nyumbani baada ya kupata nafuu.