Home » Mike Sonko Apiga Abautani kwa Sakaja!

Aliekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko (kushoto) na Gavana wa sasa Johnson Sakaja. Picha | DENNIS ONSONGO

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko amebadili msimamo wake wa kisiasa na kumuunga mkono gavana wa sasa Johnson Sakaja licha ya kumpinga tangu kuchaguliwa kwake.

Akizungumza leo, Sonko ametoa wito kwa wakazi wote wa Nairobi kumuunga mkono bosi wa sasa wa jiji.

Amesema kuwa msaada wake wa sasa umekuja baada ya kuona kuwa Sakaja pia amebadilika na kuwa bora.

Gavana huyo wa zamani alikuwa akimjibu Seneta mteule Gloria Owoba ambaye aliwahakikishia Wakenya kwamba kuondolewa kwa Sakaja madarakani kunakaribia.

Akizungumza wakati wa mahojiano runinga moja nchini, Owoba amemuonya gavana huyo akimkumbusha kuwa alichaguliwa kwa tiketi ya United Democratic Alliance (UDA).

Hapo awali, gavana huyo wa zamani alikuwa ametishia kukusanya saini za kumrudisha nyumbani Sakaja ikiwa angeendelea kuwahangaisha wafanyabiashara wa jijini Nairobi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!