Home » Stevo Simple Boy apokezwa tuzo youtube.

Stevo Simpleboy na nguo yenye msemo wake Freshi Barida.

By Burare Kennedy.

Msanii Stevo Simple Boy ametunukiwa tuzo ya silver play button na mtandao wa youtube baada ya kufikisha jumla ya subscribers laki moja kwenye channel yake.

Uongozi wake wa MIB umetumia ukurasa wake wa Instagram kuwashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wanazidi kumuonyesha kupitia kazi zake za muziki.

Channel ya youtube ya Stevo Simple Boy ilifunguliwa rasmi Machi 31 mwaka wa 2022 na mpaka sasa imefikisha zaidi ya watazamaji millioni 3.8 huku ikiwa na jumla ya subscribers 123, 000.

Itakumbukwa tuzo ya Silver Play Button huwa inatolewa kwa wanamuziki au watu maarufu kwenye mtandao wa Youtube ambao hujizolea zaidi ya subcribers laki moja.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!