Home » King Saha akanusha madai ya kutumia mihadarati.

King Saha.

By Burare Kennedy.

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda King Saha amejitenga na madai yaliyoibuliwa na Bebe Cool kuwa anatumia mihadarati.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema alihasi matumizi ya dawa za kulevya miaka mingi iliyopita baada ya kugundua kuwa inaathari afya yake.

Hitmaker huyo wa “Zakayo”, ameanika tusiyojua kuhusu Bebe Cool kwa kusema kuwa msanii huyo anatumia bangi pamoja na miraa huku akiongeza kuwa alimfunza jinsi ya kutumia dawa za kulevya kipindi cha nyuma.

Hata hivyo ametishia kumshambulia Bebe Cool iwapo hataacha tabia ya kumchafulia jina kwenye vyombo vya habari kwa kusema kuwa ana nyimbo nyingi ambazo zipo studio kwa ajili kuanika maovu yote ambayo bosi huyo wa Gagamel amekuwa akifanya kwa siri.

King Saha ambaye juzi kati aliondoka hospitalini ambako alikuwa amelazwa baada ya kuugua ugonjwa usiojulikana, atasalia nyumbani kwa wiki mbili zijazo kwa ajili kujiweka sawa kiafya.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!