Home » Mwanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja nchini Kenya akiri kuua kisa usaliti.

By Burare Kennedy.

Mwanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja (LGBTG) Nchini Jackson Odhiambo amekiri kumuua mpenzi na mume wake Edwin Chiloba kwa madai ya kumsaliti kimapenzi.

Wawili hao walikuwa wanaishi pamoja kama mke na mme kwa takribani mwaka mmoja kabla ya tukio hilo la kutisha.

Odhiambo almaarufu Lizer ambaye alikiri kuwa alilazimika kupanga mauaji hayo kwa usaidizi wa marafiki wengine wawili baada ya kugundua kuwa mpenzi Edwin Chiloba alikuwa na mahusiano na mwanamume mwingine.

Inasemekana Lizer alitumia simu ya mpenzi wake kumtahadharisha mlinzi kuwa wanahama eneo hilo, baadaye aliondoka na vitu vilivyowekwa kwenye sanduku la chuma bila kujua ni mwili wa Edwin ambao ulipatikana umbali wa kilomita 20 kutoka eneo la tukio.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!