Home » Somalia yadai al-Shabab imeomba kushiriki mazungumzo kwa mara ya kwanza.

Somalia yadai al-Shabab imeomba kushiriki mazungumzo kwa mara ya kwanza.

By Burare Kennedy.

Serikali ya Somalia imedai kwamba kwa mara ya kwanza kundi la itikadi kali la Al-Shabaab limeomba kufanya mazungumzo ya wazi, huku kukiwa na mashambulizi ya kijeshi.

Waziri wa Ulinzi Abdifatah Kasim aliwaambia waandishi wa habari mjini Mogadishu kwamba kundi hilo limejumuisha wenyeji na wageni, na Wasomali wa kundi hilo wana nafasi ya mazungumzo, lakini wageni waliovamia nchi hiyo hawana haki ya mazungumzo na chaguo pekee ni kurudi walikotoka.

Hata hivyo hakuna tamko lolote kutoka kwa al-Shabab, kundi ambalo kwa zaidi ya muongo mmoja limefanya mashambulizi makubwa ya mabomu katika mji mkuu wa Somalia na sehemu zinazodhibitiwa za mikoa ya kati na kusini mwa nchi, na kutatiza juhudi za kujenga upya taifa hilo baada ya miongo kadhaa ya migogoro.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!