Home » Rais Ruto Aondoka Nchini

Rais William Ruto ameondoka nchini jana Jumatano usiku kwa ziara ya siku tatu katika Mataifa ya Comoro na Jamhuri ya Kongo.

 

Katika taarifa kwa vyumba vya habari, msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed amesema hii leo Alhamisi, Julai 6, 2023, Rais Ruto atakuwa mgeni mkuu wakati wa maadhimisho ya miaka 48 ya Uhuru wa Muungano wa Comoro, kwa mwaliko wa Rais Azali Assoumani.

 

Ijumaa, Julai 7, Rais Ruto ataanza ziara ya Kiserikali ya siku mbili katika Jamhuri ya Kongo ambapo ameratibiwa kufanya mazungumzo baina ya nchi hizo mbili na Rais Dennis Sassou Nguesso akiangazia ushirikiano wa kimkakati wa Kenya na Kongo.

 

“Wakuu wa Nchi pia watashuhudia utiaji saini wa hati za kisheria kuhusu mikataba mbalimbali ya nchi hizo mbili. Kenya na Kongo zinafurahia uhusiano wa kindugu uliojengwa juu ya urafiki na ushirikiano wa muda mrefu katika ngazi za nchi mbili, kikanda na kimataifa,” aliongeza msemaji wa Ikulu.

 

Ziara ya Ruto nchini Kongo inafuatia kikao cha uzinduzi wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Kenya na Kongo, ambacho kilifanyika na maafisa kutoka nchi zote mbili kati ya Juni 25 na Juni 27, 2023.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!