Home » Mwanaume Amuua Mkewe Kwa ‘Kuuza Maharagwe Bila Idhini Yake’

Mwanaume Amuua Mkewe Kwa ‘Kuuza Maharagwe Bila Idhini Yake’

Polisi katika Kaunti ya Kirinyaga wamemkamata mwanamume mmoja kutoka kijiji cha Gichonjo, ambaye anadaiwa kumdunga kisu mkewe hadi kufa kutokana na uuzaji wa maharagwe bila kushauriana naye.

 

Wakaazi walisema kuwa wawili hao walikuwa wamevuna maharagwe hayo pamoja na mwanamume huyo aliporudi nyumbani alianza kupigana na mkewe, akamuua na baadaye kujisalimisha katika kituo cha polisi cha Kianyaga.

 

Mauaji hayo yalizua taharuki kubwa miongoni mwa wakazi waliokuwa wakitafuta damu yake baada ya tukio hilo.

 

Wakaazi wa eneo hilo walisema kuwa walipata mwili huo ukiwa umelala sakafuni jikoni kwenye dimbwi la damu ishara tosha kwamba alikuwa amedungwa kisu mara kadhaa.

 

Polisi walisema kuwa mshukiwa, 40, anashikiliwa huku wakianza uchunguzi kubaini kilichosababisha mauaji hayo.

 

Mwili wa marehemu ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Kerugoya level 5 ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!