Home » KNBS: Murang’a, Narok Zaongoza Kwa Ngono Nje Ya Ndoa

Asilimia 19 ya wanawake na 35% ya wanaume kati ya umri wa miaka 15-49 wamefanya ngono na mtu ambaye hakuwa mume, mke, au mwenzi wao wa kuishi pamoja katika miezi 12 iliyopita.

 

Haya ni kwa mujibu wa Utafiti wa Demografia na Afya nchini (KDHS) 2022 unaoonyesha kuwa 37% ya wanawake hao wametumia kinga wakati wa kujamiiana huku asilimia ya wanaume ikifikia 68%.

 

Ripoti hiyo pia inaongeza kuwa asilimia ya wanawake walio katika mabano sawa huongezeka kulingana na kiwango cha utajiri kwani 14% walitangamana na wenzi kutoka kiwango cha chini huku 22% wakichagua wale walio katika kiwango cha juu zaidi.

 

Kiwango cha elimu pia kilikuwa kigezo cha kuchagua mwenza kwani 7% ya wanawake walitangamana na wasio na elimu na 27% walitangamana na wale walio na elimu ya sekondari na zaidi.

 

Vile vile, mtindo huo huo ulionekana kwa wanaume kwani 20% walitangamana na watu wasio na elimu ikilinganishwa na 43% waliochagua washirika wa elimu ya sekondari na zaidi.

 

Kaunti ya Murang’a ilirekodi asilimia kubwa zaidi (11%) ya wanawake ambao walikuwa na wapenzi 2 au zaidi katika muda wa miezi 12 iliyopita, huku kaunti zilizo na asilimia ndogo zaidi ni kaunti za Mandera, Tana River na Kwale zenye chini ya 1% kila moja.

 

Kaunti ya Narok ina asilimia kubwa zaidi (43%) ya wanaume ambao walikuwa na wapenzi 2 au zaidi katika muda wa miezi 12 iliyopita, huku kaunti za Kirinyaga, Kericho na Garissa zikiwa na asilimia ndogo zaidi zikiwa na 2% kila moja.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!