Home » Koigi: Udikteta Umerejea Nchini

Mbunge Wa Zamani Wa Subukia Koigi Wa Wamwere Sasa Amesema Kuwa Suala Zima La Korti Kusimamisha Utekelezwaji Wa Mswaada Mpya Wa Fedha Wa Mwaka Wa 2023 Ambao Tayari Umetiwa Saini Na Rais Ruto Kuwa Sheria Ni Ishara Tosha Kwamba Uongozi Wa Kidikteta Humu Nchini Kulingana Na Yeye Umeingia Dosari.

 

Ansema Itakuwa Vigumu Kwa Serikali Kupuuzilia Mbali Kauli Ya Mahakama Kwani Rais Ruto Hapo Awali Alikuwa Ameshasema Serikali Yake Itaheshimu Amri Zote Za Mahakama Humu Nchini.

 

Kogi Vile vile Amesema Kuwa Serikali Ya Kenya Sasa Inadhihirisha Wazi Kuwa Ni Serikali Ya Mabwenyenye Kinyume Na Ilivyokuwa Ikitarajiwa Na Wakenya Hapo Awali Kabla Ya Uchaguzi Wa Mwaka Jana Kwenye Kampeini.

 

Kiongozi Huyo Wa Zamani Sasa Anasema Viongozi Wa Kenya Kwanza Imewasaliti Wakenya Kwani Watoto Wao Ndio Sasa Wananufaika Pakubwa Na Uongozi Wao Kinyume Na Matarajio Ya Wengi.

 

Kwa Upande Wake Mwangu Njui Kwa Upande Wake Amesema Kuwa Huu Ndio Wakati Wa Serikali Kuangazia Mahitaji Ya Wananchi Na Wala Sio Kuongeza Ushuru Unaopania Kuwekezwa Kwenye Miundomisingi Ambayo Haitawafaidi Wananchi Ambao Wanapitia Mahangaiko Wakati Huu Ambapo Gharama Ya Maisha Imepanda Mara Dufu

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!