Home » Azimio Yakashfu Kenya Kwanza

Viongozi Wa Muungano Wa Azimio La Umoja Wameikashifu Serikali Kutokana Na Kutozwa Ushuru Wa Juu Huku Kukiwa Na Gharama Kubwa Ya Maisha.

 

Akizungumza Wakati Wa Hotuba Ya Hadhara Mjini Kitale Aliyekuwa Waziri Wa Ulinzi (Cs) Eugene Wamalwa Alisema Kuwa Serikali Imethibitisha Kutojali Wakenya Kwa Kuweka Viwango Vya Kikatili Vya Kutoza Ushuru Katika Sheria Ya Fedha Ya 2023 Bila Kuzingatia Hali Mbaya Iliyopo.

 

Wamalwa Vilevile Aliwakashifu Vikali Wabunge Wa Upande Wa Azimio Waliounga Mswaada Huo Bungeni Na Kuwataja Kama Wasaliti Wanaoupunja Juhudi Za Upinzani Nchini.

 

Kwa Upande Wake, Mbunge Wa Saboti Caleb Amisi Alitupilia Mbali Ushuru Wa Makazi Uliopendekezwa Na Serikali, Akibainisha Kuwa Sio Muhimu Kwa Wakenya Na Ni Vyema Serikali Kuelekeza Nguvu Katika Kupunguza Uchumi Unaoporomoka.

 

Ikumbukwe Kuwa Mswada Wa Fedha Uliidhinishwa Kuwa Sheria Na Rais Ruto Mnamo Juni 26 Baada Ya Kupitishwa Katika Bunge La Kitaifa.

 

Haya Yanajiri Huku Amri Mbili Za Mahakama Zikiwa Zimetolewa Na Mahakama Kuu Kusitisha Utekelezaji Wa Sheria Ya Fedha Ya 2023 Baada Ya Maombi Yaliyowasilishwa Na Seneta Wa Busia Okiya Omttata Na Peter Agoro, Wakidai Kuwa Mswada Huo Uliasisiwa Kwa Uharamu Na Hivyo Kukiuka Katiba.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!