Home » Madaktari Watishia Kugoma

Madaktari wa Huduma ya Afya kwa Wote (UHC) wametishia kugoma ikiwa mizozo yao ya uajiri kati ya Kaunti na Serikali ya Kitaifa haitatatuliwa.

 

Wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Muungano wa Kitaifa wa Wanateknolojia wa Dawa nchini, Mutuma E. Irura, wafanyikazi wa matibabu wamesema kuna ukosefu wa viwango katika kaunti na serikali imeendelea kupanga kutoa mafunzo kwa wafanyikazi bila mipango ifaayo ya kuajiriwa.

 

Aliongeza kuwa hali hiyo imewaacha zaidi ya wafanyikazi 8,000 wa UHC wakihangaika tangu Mei 2023 jambo ambalo limehatarisha pakubwa tija yao kwani Wizara ya Afya imeshindwa kutoa maagizo mwafaka ya sera kwa serikali ya kaunti.

 

Aidha Wameshutumu Baraza la Magavana kwa kuwakana wafanyikazi wa UHC wakisema mwenyekiti ameendelea kufanya dhihaka kwa wafanyikazi wa afya.

 

Sasa wanatoa wito kwa serikali ya Kitaifa na Kaunti kwa usaidizi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!