Home » Kenya, Ufaransa Zakubali Kushirikiana

Serikali ya Kenya imefikia makubaliano na Ufaransa kuchangia kwa pamoja rasilimali ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kama suala la kimataifa.

 

Rais William Ruto, ambaye amezungumzahii leo Ijumaa wakati wa kuhitimisha mkutano wa kilele wa ‘How Dare You’ mjini Paris, alisema mataifa hayo mawili yaliazimia kukabiliana na changamoto ya hali ya hewa bila kujali maslahi ya kipekee ya nchi.

 

Rais alisisitiza kwamba hakuna nchi inapaswa kupuuza athari za hali ya hewa ikiwa imeathiriwa au la, na kuongeza kuwa msingi wa utajiri wa taifa au umaskini haupaswi kuwa kikwazo cha kupambana na athari.

 

Rais Ruto alirejelea matamshi ya awali ya Waziri Mkuu wa Barbadia Mia Motley ambapo alihimiza mataifa kuweka kando maslahi ya kibinafsi kama njia ya kuungana ili kukabiliana na mzozo wa kimataifa, akisisitiza kwa washikadau kushirikiana katika kuwahakikishia mafanikio.

 

Kuhusu Mkutano ujao wa Kilele wa Hali ya Hewa barani Afrika uliopangwa kufanyika Septemba 4 – 6, 2023 jijini Nairobi, rais alidai kwamba haikuchelewa kwa mkutano huo kupiga hatua muhimu katika kuhakikisha mabadiliko makubwa yameafikiwa kabla ya wakati huo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!