Home » Babu Owino Adai Ametumia Ksh.58.6M Kumtibu DJ Elvole
Babu says he has spent 58.6M on DJ Evolve

Embakasi East MP Babu Owino Photo courtesy

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amesema kuwa ametumia shilingi Milioni 58.6 kutibu na kutunza bili zote za Felix Orinda almaarufu DJ Elvolve.

 

Haya yanajiri kufuatia kesi inayoendelea mahakamani inayomhusisha na shtaka la kumpiga risasi Felix Orinda almaarufu DJ Evolve mnamo Januari 2020.

 

Alipokuwa akijitetea katika kesi ambapo alipatikana na kesi ya kujibu kuhusu matumizi mabaya ya bunduki, Babu Owino alimweleza hakimu wa mahakama Bernard Ochoi kwamba alinunua Ksh. Ghorofa ya shilingi Milioni 17 kwa ajili ya DJ huyo katika eneo la Kilimani jijini Nairobi anakoishi kwa sasa.

 

Vile vile mahakama ilisikia kwamba ana mipango ya kumpeleka DJ Evolve kwa matibabu zaidi na kumfungulia DJ huyo biashara ya akademi Wakati wa shauri hilo, mbunge huyo aliiambia mahakama kuwa siku hiyo bunduki yake ilikwama na hivyo hakuna uwezekano kuwa ndiyo iliyofyatua risasi.

 

Kesi yake imeahirishwa kwa ajili ya kusikilizwa tarehe 22 Juni 2023.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!