Home » Matarajio Ya Bajeti Yapanda Hata Zaidi

Ili kufadhili bajeti ya mwaka wa Fedha wa 2023/2024 ya shilingi trilioni 3.6, hazina ya kitaifa imependekeza msururu wa hatua za kodi kama ilivyo kwenye Mswada wa Fedha wa 2023, uliopitishwa Jumatano na Bunge.

 

Miongoni mwa vifungu katika muswada huo ni pendekezo la kuoanisha Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa mbalimbali zikiwemo za mafuta ya petroli.

 

Hata hivyo, washikadau katika sekta ya uchukuzi wameelezea hofu kwamba ikitekelezwa, ushuru wa asilimia 16 wa VAT kwa bidhaa za petroli utakandamiza biashara na kuzorotesha hali yao ya kiuchumi.

 

Petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa sasa yanauzwa kwa bei ya wastani ya juu ya shilingi 182, 167, na 161 mtawalia.

 

Hatua hii inatokana na malipo ya sasa ya VAT ya asilimia 8 Bei hizi hata hivyo zinatarajiwa kupanda iwapo pendekezo la kuongeza maradufu ya asilimia 8 ya VAT inayotozwa kwa sasa kwenye bidhaa za mafuta kama ilivyo katika Mswada wa Fedha wa 2023 litatekelezwa pindi mswada huo utakapoidhinishwa kuwa sheria bila marekebisho.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!