Jinsi Felicity Shiru Aelezea Alivyoshughulikia Kashfa Dhidi Ya Thee Pluto
YouTuber na mfanyabiashara Robert Ndegwa almaarufu thee Pluto hivi majuzi alifichuliwa na mwanablogu fulani kwa madai ya kumsaliti mpenzi wake.
Mwanablogu huyo aitwaye Njambi alishiriki screen shot za mazungumzo na mwanamke ambaye alisema alikuwa na wakati wa karibu na Thee Pluto huko Mombasa na akamlipa sh10,000 ili anyamaze.
Hata hivyo, mpenzi wa Felicity, Thee Pluto amemtetea.
“I think Pluto ndio alinionyesha aish sasa huyu dame ni nini?”
“Mi hata akili zangu haziko huko nilikuwa like what are those, ni nini. Unajua ukimwamini mwenzako kuna vitu tuu unaona hata havina maana. Na pia kwa upande wangu nadhani kuna mtu aliniDM’d. akiniambia ati unajua mpenzi wako anadanganya vitu ka hizo.”
Felicity aliongeza kuwa alifahamishwa kabla ya kashfa ya ulaghai kuzuka, lakini haikuwa wazi juu ya utambulisho wa mdokezi.
“Sijui kama ni mtu yule yule wa stori sijui. Lakini kuna mtu alinitumia meseji akisema unajua mpenzi wako anacheat”
Felicity hakuwahi mwambia Thee Pluto kuhusu taarifa za faragha alizopokea akieleza kwa nini
“By the way sikuambia Pluto sikuwa naona ikimake sense.”
Inavyoonekana, mdokezi alimuuliza Felicity kama anataka uthibitisho kuwa babake mtoto anadanganya “akaniuliza unataka risiti? Mi nikamwabia tuu nikicheka tuma kaa unataka kama” Felicity aliendelea.
Mdokezi huyo alidaiwa kutoweka na hakutuma ushahidi waliodai kuwa nao wa Thee Pluto kudanganya.
“Aka vanish later on ndo Thee Pluto akakuja akanishow kwa stori stoy zake sijui nini nini”
“Kwa hivyo, bila shaka, alijaribu na kunielezea kila kitu kama lazima tueleze, unajua sisi ni kitu na sote.”
Mazungumzo kati ya wanandoa hao yalipelekea kuhitimisha kuwa ni mtu aliyetaka kuchafua jina la Thee Pluto.
“Tangu kumekuwa na stori kuhusu yeye sijui za kuscam na hayo yote tangu wakati huo nadhani kuna baadhi ya watu wamekuwa wakijaribu kumwangusha.”
“Nikiangalia mantiki jinsi Pluto alivyonieleza kila kitu ilikuwa na maana. Coz najua alipo, vitu kaa hizo so that whole story didn’t make any sense.”