Home » SUPKEM Yaikosoa Serikali Kuhusu Vifo Vya Shakahola

Supreme Council of Kenya Muslims (SUPKEM) Photo courtesy

Baraza Kuu la Waislamu wa Kenya (SUPKEM) limeinyooshea kidole serikali kwa kile wanachotaja kuwa ulegevu katika kuweka hatua kali za kuwadhibiti viongozi walaghai wa kidini dhidi ya kuwahadaa wafuasi wao.

 

Wakiwasilisha maoni yao kwa Kamati ya Seneti ya AdHoc, walisema kwamba ikiwa kungekuwa na mifumo ya udhibiti ambayo mtu yeyote anayefundisha mafundisho angefanya kazi, basi dhehebu la Shakahola, ambapo watu 274 wamethibitishwa kufa hadi sasa lingeweza kuepukika.

 

Ili kuzuia matukio hayo yasijirudie, Sheikh Hasaan alipendekeza ziundwe kamati za walinda milango ili kudhibiti na kusimamia vyombo vya kidini.

 

Kwa sasa serikali inachunguza vifo hivyo pamoja na madai ya kuteswa na kuwatendea kinyama wafuasi wa kasisi mwenye utata Paul Mackenzie na kanisa lake la Good News International lenye makao yake makuu katika Kaunti ya Kilifi.

 

Mchungaji Mackenzie yuko kizuizini cha siku 30 kilichoanza Mei 10, pamoja na washukiwa wengine 17 akiwemo mkewe ambao walifikishwa katika mahakama za Shanzu.

 

Washukiwa hao wanazuiliwa katika vituo mbalimbali vya polisi kote Kilifi huku uchunguzi kuhusu vifo vya watu hao ukiendelea.

 

Wakati uo huo, idadi ya wahasiriwa ambao wametambuliwa na jamaa zao bado imesalia 19 wakati ambao bado hawajapatikana ni 613.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!