Home » Bodi Ya Barabara Nchini Kenya Yataka Kukusanya Ksh. 512B

Bodi Ya Barabara Nchini Kenya Yataka Kukusanya Ksh. 512B

Bodi ya barabara nchini Kenya inapanga kukusanya shilingi bilioni 512 zitakazotumika katika ujenzi wa kilomita 220,000 za barabara nchini katika muda wa miaka 5 ijayo.

 

Bodi hiyo pia inatafuta kujenga njia za kutembea kwa watumiaji wa miguu katika miji yote mikuu ili kupunguza ajali na kuimarisha usalama wa watembea kwa miguu.

 

Akizungumza wakati wa kuzindua rasmi mpango mkakati wa Bodi ya Barabara ya Kenya kwa miaka ya 2023 hadi 2027, mkurugenzi mkuu wa wakala wa barabara, Rashid Mohammed amesema kuwa chini ya mpango huo wa kimkakati, angalau asilimia 84 ya barabara zote nchini zitakuwa katika hali nzuri.

 

Waziri wa Uchukuzi na Miundombinu, Kipchumba Murkomen, alisema wizara yake itakuja na gharama nzuri za barabara kwa magari ya umeme huku serikali ikiendelea na harakati za uhamaji wa umeme.

 

Itakumbukwa kwamba katika siku za hivi karibuni visa vya ajali vimeongezeka nchini huku wakenya wengi wakidai kwamba ni miundomisingi mibovu iliyochangia.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!