Home » KNBS:Pengo Baina Ya Matajiri Na Maskini Lazidi Kupanuka

Pengo kati ya matajiri na maskini wa Kenya imeendelea kukua katika kiwango cha juu katika kipindi hiki cha hali ngumu ya kiuchumi.
Haya ni kulingana na ripoti ya Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu (KNBS) ambayo ilifichuliwa kwa umma Alhamisi.

 

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa idadi ya umaskini kwa ujumla imekithiri zaidi katika maeneo ya vijijini ikifikia asilimia 40.7 ikilinganishwa na maeneo ya mijini ambayo yana asilimia 34.1.

 

Umaskini uliokithiri bado ni mkubwa katika maeneo ya vijijini, ambapo asilimia 7.8 ya wakazi sawa na (watu milioni 2.6) walikuwa maskini 34 ikilinganishwa na maeneo ya mijini ambako asilimia 1.5 ya wakazi walikuwa maskini wa kupindukia.

 

Kulingana na ripoti hiyo, jamii milioni 4.4 kitaifa zinaishi katika umaskini kwa ujumla.

 

Kaunti sita zilizo na pengo kubwa la umaskini ni pamoja na Turkana (38.2%), Wajir (26.6%), Samburu (25.9%), Mandera (25.2%), Marsabit (20.7%) na Tana River (20.5%).

 

Ripoti hiyo baadaye inabainisha kuwa kiwango cha umaskini wa watu binafsi katika ngazi ya kitaifa kilikuwa asilimia 5.8, ikimaanisha kuwa watu milioni 2.8 wanaishi katika hali ya umaskini uliokithiri na hawakuweza kumudu chakula kila siku.

 

Ripoti hiyo pia imefichua hali ya kusikitisha ya hali ya chakula katika kaunti ikizingatia kwamba watu milioni 10.8 wako chini ya mstari wa umaskini wa chakula.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!