Home » Naibu Rais Gachagua Awarai Wabunge Kuwa Na Nidhamu

Naibu rais Rigathi Gachagua amewataka wabunge kufanya shughuli za Bunge kwa heshima baada ya kushambuliwa kwa mbunge mteule Sabina Chege kwa madai ya kutong’atuka katika uongozi wa wachache bungeni.

 

Hiyo jana wabunge saba wa Azimio walipigwa marufuku ya kuhudhuria vikao vya bunge kwa siku tano na majuma mawili kwa kukosa nidhamu wakati wa vikao wengi wakitaja marufuku ya muda kama njama ya serikali kuhakikisha Mswada tata wa Fedha 2023 unapitishwa.

 

Wabunge Kadha walipewa marufuku ya majuma mawili, na wengine siku tano kufuatia vurugu zilizozuka kati ya wabunge wa Azimio la Umoja-One Kenya na Kenya Kwanza, Azimio ikishikiniza kubanduliwa kwa mbunge maalum Sabina Chege kama naibu kiranja wa wachache bungeni.

 

Waliopitia shoka hilo ni pamoja na Mbunge wa Kisumu Magharibi Rosa Buyu, Bi Millie Odhiambo (Suba Kaskazini), TJ Kajwanga wa Ruaraka, Catherine Omanyo (Busia), Joyce Kamene (Machakos), Amina Mnyazi wa Malindi, na Sabina Chege mwenyewe.

 

Wetangula alisusia kumbandua Bi Sabina, akihoji “amefungwa mikono na amri ya korti”.

 

Jubilee ilimfurusha mbunge huyo maalum kama kiongozi wa chama.

 

Upinzani, unaoongozwa na kinara wa Azimio, Raila Odinga umeapa kutumia mbinu zote kuangushwa Mswada wa Fedha 2023 unaopendekeza nyongeza ya ushuru (VAT), ikiwemo ya mafuta na asilimia 3 ya mshahara wa kila mfanyakazi kukatwa kwa minajili ya mpango wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu.

 

Wengi wa Wakenya, mashirika na vyama kutetea wafanyakazi wanapinga mswada huo unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni kujadiliwa kupitishwa au kuangushwa kabla Makadirio ya Bajeti 2023/24 kusomwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!