Home » Bungoma: Polisi Avamiwa Na Umati Kwa Madai Ya Kuiba Ng’ombe

Bungoma: Polisi Avamiwa Na Umati Kwa Madai Ya Kuiba Ng’ombe

Afisa wa polisi katika eneo bunge la Lugari Bungoma alivamiwa na kundi la watu kwa madai ya kuhusika na wizi wa mifugo katika eneo hilo.

 

Afisa huyo wa polisi anadaiwa kuiba ng’ombe na kumsafirisha mnyama huyo kwa kutumia land cruiser ya polisi hadi kaunti nyingine.

 

Kulingana na wakaazi ndani ya eneo hilo kinyesi cha ng’ombe kilipatikana kwenye gari la afisa huyo wakiwa kwenye eneo la kuosha magari.“Gari la polisi lilikuwa na kinyesi cha ng’ombe hivyo ilinishangaza. Inakuwaje gari la polisi lilikuwa na kinyesi cha ng’ombe?,” mkazi mmoja alisema.

 

Uwepo wa kinyesi cha ng’ombe ndani ya gari ulitosha kwa wakazi kuwapunguza washukiwa wao kwa afisa aliyekuwa akiendesha gari hilo.

 

Benson Somek, mwendesha boda-boda katika eneo hilo alishutumu watekelezaji sheria kwa kuwa wahusika wakuu wa vitendo vya uhalifu.

 

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Lugari Bernard Ngungu alisema kuwa uchunguzi utafanywa na hatua mwafaka za kisheria zitachukuliwa.

 

“Iwapo afisa wetu atabainika kuhusika na suala hilo, tutachukua hatua za kiutawala. Huenda alichukua gari bila kibali hivyo tutamshughulikia idara,” alisema.

 

Ng’ombe huyo aliyeibwa aligunduliwa katika mji wa Webuye, kaunti ya Bungoma

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!