Mudavadi Awasuta Wapinzani Kwa Kupotosha Wakenya
Waziri Mkuu Musalia Mudavadi amewataka wakosoaji wa Mswada wa Fedha wa 2023 kuipa serikali njia mbadala za kukusanya mapato katika mwaka ujao wa kifedha.
Mudavadi amesema hali ambayo nchi iko kwa sasa inayohitaji maamuzi magumu ambayo mengine yatakuwa machungu kwa muda mfupi lakini yenye manufaa kwa muda mrefu.
Alisema hayo katika ukumbi wa Bomas of Kenya alipohutubia wanachama wa Chama cha Kitaifa cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda nchini.
Amewataka wajumbe wa baraza hilo kuunga mkono serikali katika kubadilisha mjadala wa sasa wa Muswada wa Sheria ya Fedha wa 2023, akisema serikali ina maana nzuri kwa wananchi.
Vile vile amewataka wanachama wa chama hicho kuwapa Wakenya picha halisi ya kile kinachokusudiwa.
Mudavadi ametetea mapendekezo ya ushuru wa nyumba akisema wazo hilo limepotoshwa na limetiwa siasa ili kuwafanya Wakenya wahisi kama Serikali inawatwika mzigo.