Home » Watu Kadhaa Wakamatwa Wakipinga Mswada Wa Fedha Jijini Nairobi

Watu Kadhaa Wakamatwa Wakipinga Mswada Wa Fedha Jijini Nairobi

Wapigania haki yaandamana dhidi ya mswada wa fedha 2023 jijini Nairobi Picha:AFP

Waandamanaji kadhaa waliojitokeza katika barabara za Nairobi kupinga mapendekezo ya Mswada wa Fedha wa 2023-24 wamekamatwa.

 

Waandamanaji hao waliobeba mabango ya kulalamikia gharama ya juu ya maisha na ushuru walitaka Mswada wa Fedha utupiliwe mbali.
Walikutana na ulinzi mkali wa maafisa wa polisi waliovalia kiraia na sare ambao waliwakamata baadhi yao.

 

Mswada huo ambao tayari uko katika Bunge la Kitaifa ukisubiri uamuzi wa wabunge, umekuwa ukikosolewa vikali na viongozi na Wakenya vile vile.

 

Rais William Ruto aliwataka wabunge wa Kenya Kwanza kuipitisha huku kiongozi wa upinzani Raila Odinga akiwataka wabunge wa Azimio kuikataa.

 

Kesi imewasilishwa kupinga kupitishwa kwake na itasikilizwa Juni 19.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!