Home » Kiraitu Amshauri Rais Ruto Jinsi Ya Kutatua Mzozo Wa Madeni

Kiraitu Amshauri Rais Ruto Jinsi Ya Kutatua Mzozo Wa Madeni

Mwenyekiti wa Shirika la Kitaifa la Mafuta nchini Kenya Kiraitu Murungi amemtaka Rais William Ruto kuwekeza katika uzalishaji wa mafuta akisema hilo ndilo jibu la mzozo wa madeni uliopo.

 

Amesema nchi inaweza kupata zaidi ya dola bilioni 8 kutoka kwa eneo la uchimbaji mafuta la Lokichar pekee kule Turkana, pesa ambazo amesema zitatosha kupunguza utegemezi wa misaada na kuwaondoa mamilioni ya Wakenya kutoka kwa umaskini.

Shirika la Tullow mnamo Mei iliwasilisha Mpango wake wa Maendeleo ya Uwanda uliorekebishwa kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli na sasa inakaguliwa.

 

Murungi, aliyekuwa waziri wa Nishati, amekashifu utawala wa Uhuru kwa kupuuza sekta ya mafuta licha ya rasilimali hiyo ya thamani kugunduliwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.

 

Nchi zilizoshiriki katika mkutano huo ni Norway, Somalia, Tanzania, Zanzibar, Uganda, Angola, Msumbiji, Ghana na Afrika Kusini na Kenya.

 

Murungi alisema ufunguo wa uhuru wa nishati barani Afrika na mabadiliko ya haraka ya kijamii na kiuchumi ni unyonyaji endelevu wa rasilimali kubwa ya mafuta na gesi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!