Home » Gachagua: Mswada Wa Fedha Utapitishwa Tu

Naibu Rais Rigathi Gachagua amesisitiza kuwa Mswada wa Fedha wa 2023 lazima upitishwe jinsi ulivyo.

 

Akizungumza wakati wa hafla ya harambee katika Shule ya Sekondari ya St Charles Lwanga huko Kitui hii leo Jumamosi, Naibu Rais amesema mswaada huo haulengi kukandamiza wakenya kama baadhi ya viongozi wa upinzani wanavyodai bali ni kuunda ajira kwa vijana wa humu nchini.

 

Gachagua amemkashifu kiongozi wa Azimio, Raila Odinga, aliyetaka muswada wa Sheria ya Fedha wa 2023 uondolewe kabisa, akisema mswaada huo utapita bila kupingwa kwani serikali ya Kenya kwanza ina idadi ya wabunge wengi kuupitisha mswaada huo.

Mbunge wa Kitui Mashariki Nimrod Mbai, ambaye alikuwa kwenye hafla hiyo, amesema yeye kama kiongozi anaona mswaada huo ushapita kitambo bila pingamizi yoyote.

 

Seneta Mteule Tabitha Mutinda, kwa upande wake, alisema Mswada wa Fedha una vitu ‘vizuri’ vingi.

 

Hata hivyo, Mbunge wa Kitui ya Kati Makali Mulu alisema hakuna nchi ambayo imewahi kuwatoza watu wake ushuru kwa ustawi, na kuongeza kuwa Mswada huo unapaswa kupigwa chini.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!