Home » Machafuko Yashuhudiwa Wakati Wa Usajili Wa Chama Cha UDA Marsabit

Machafuko Yashuhudiwa Wakati Wa Usajili Wa Chama Cha UDA Marsabit

Machafuko Marsabit wakati wa usajili wa UDA Picha:Kenyans.co.ke

Machafuko yamekumba zoezi la usajili wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) katika ukumbi wa Catholic Hall katika Kaunti ya Marsabit hii leo Jumamosi .

 

Kwa mujibu wa taarifa za awali, machafuko hayo yalisababishwa na makundi hasimu yanayopigania kutambuliwa katika Chama cha UDA.

 

Kufuatia mapigano hayo, maafisa wa polisi waliotumwa kurejesha amani walilazimika kufyatua vitoa machozi katika makundi yanayopigana kwa lengo la kurejesha utulivu.

 

Katibu Mkuu wa UDA Cleophas Malala alikuwa ameandaa zoezi la usajili mashinani katika kaunti hiyo lakini alizomewa na vijana alipokuwa akitoa hotuba ya kuwalazimisha maafisa wa sheria kuingilia kati.

 

Baada ya utulivu kurejea, Malala aliahidi kushughulikia sintofahamu hiyo inayovikutanisha vikundi pinzani.

 

Malala aliwaambia wakazi kuwa UDA itachagua viongozi watakaowakilisha Marsabit kulingana na watu watakaosajiliwa.

 

Hata hivyo, haikuwa wazi kwa nini makundi hayo mawili yalikuwa na mzozo.

 

Licha ya fujo na usumbufu, Malala alitangaza kuwa UDA ilipanga kusajili angalau watu milioni 15.

 

Seneta huyo wa zamani wa Kakamega alidokeza kuwa wanachama hao wapya walikuwa muhimu kumpa Ruto mamlaka zaidi na msingi.

 

Licha ya ahadi za Malala, mkutano huo baadaye ulilazimika kumalizika mapema kwa sababu vijana waliendelea kuimba majina ya wanasiasa wanaohasimiana.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!