Tharaka Nithi: Kijana Amkata Kichwa Mama Mkwe
Polisi katika kijiji cha Karimba Kanyoni, kaunti ndogo ya Chiakariga kaunti ya Tharaka Nithi wamemkamata mwanamume mwenye umri wa miaka 22 anayeaminika kumkata kichwa mama mkwe wake mwenye umri wa miaka 46.
Akithibitisha kisa hicho, Naibu Kamishna wa kaunti hiyo Chalo Kaloki amebainisha kuwa walipokea taarifa kutoka kwa wakazi wa eneo hilo.
Kaloki anashuku kuwa huenda kulikuwa na ugomvi wa kinyumbani uliosababisha kisa hicho cha kusikitisha.
Katika tukio la asubuhi, mshukiwa anasemekana kumdunga kisu marehemu mara kadhaa kabla ya kumkata kichwa.
Mamake marehemu aliyetambulika kwa jina la Ann Karigu amebainisha kuwa aliamka na mayowe kutoka kwa bintiye muda mfupi baada ya kutoka nyumbani kukamua ng’ombe.
Anasema kwamba alishuhudia mwanamume huyo akimuua maisha ya bintiye Baadaye, mshukiwa alitishia kumuua pia.
Walioshuhudia wameambia polisi kuwa mshukiwa alielekea kazini baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama na kukamatwa na polisi na sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi.
Wakati uo huo, mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Marimanti Level Four kusubiri uchunguzi wa maiti.