Home » Gachagua Azuru Ukambani
Gachagua Azuru Ukambani

Naibu rais Rigathi Gachagua Picha: Rigathi Gachagua (Twitter)

Naibu Rais Rigathi Gachagua hii leo Jumamosi ameelekea kukutana na viongozi kadhaa katika ngome ya Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kwa ajili ya kuchangisha pesa.

 

Hii ni mara ya kwanza kwa Gachagua kuendesha harambee ya wazi tangu aingie madarakani mwezi Septemba mwaka jana katika ngome za upinzani.

 

Harambee hiyo inafanyika katika Shule ya Sekondari ya St Charles Lwanga eneo la Makali Mulu la Kitui ya Kati.

 

Mulu ni mbunge wa Wiper anayehudumu kwa muhula wake wa tatu.

 

Miongoni mwa maafisa wa serikali wanaoandamana na Gachagua ni pamoja na Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu na mwenzake wa Utalii Peninah Malonza.

 

Vile vile Baadhi ya wabunge wanahudhuria hafla hiyo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!