‘Siko Sawa’:Muigizaji Wa Zamani Wa Machachari Baha Asema
Muigizaji wa zamani wa Machachari Tyler Mbaya almaarufu Baha ameibua wasiwasi baada ya kutangaza kuwa yupo kwenye hali mbaya kimaisha.
Baada ya kufichuliwa kwa kukopa pesa kutoka kwa watumiaji mbalimbali wa Instagram, Baha aliingia kwenye mtandao wake wa InstaStories na kufunguka kuhusu masaibu yake lakini hakuweka wazi anapambana na nini.
Pia alitangaza kwamba akaunti zake za mitandao ya kijamii -Instagram na Tiktok zenye wafuasi zaidi ya 760K na 399.8K- mtawalia – zinauzwa.
Mnamo Ijumaa, Juni 2, 2023, mtumiaji wa Instagram aliyetambulika kama Nurse_Judy_ke alifichua mawasiliano yake na Baha akimsihi amtumie pesa akisema walikuwa wakikaribia kufukuzwa.
Baada ya kumtumia pesa mara kadhaa, Judy aliwasiliana na mke wa Baha Georgina Njenga ambaye alionekana kutofahamu kile mumewe alikuwa akifanya.
Mke wa Baha anasema amekuwa akilipa bili zao zote na anafichua kuwa mumewe anaweza kuwa na uraibu wa kucheza kamari zaidi.
“Sijui chochote cha aina hiyo na hapana hatufukuzwi. Hakuniambia hata juu ya hii. na ninalipa bili zote. Amekuwa akipata shida ya dau lakini ikiwa kuna chochote hakukopa pesa. kutusaidia kwa lolote pengine kwa ajili yake. Najisikia vibaya sana kwamba anatumia mtoto wetu kupata pesa na kubeti tu,” sehemu ya screenshot kati ya mazungumzo ya Judy na Georgina ilisoma.
Wakati uo huo, huenda matatizo yakazuka kati ya wanandoa hao wachanga waliopata binti mmoja baada ya mashabiki kugundua kuwa wali-unfollow kila mmoja wao kwenye mitandao ya kijamii.