Home » Msajili Wa Vyama Akataa Azma Ya Uhuru

Msajili wa Vyama vya Kisiasa amekataa kuthibitisha mabadiliko katika chama cha Jubilee ambayo yalifanywa na mrengo wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

 

Kambi ya Rais huyo wa zamani ilikuwa Mei 22 ilifanya Kongamano la Wajumbe wa Kitaifa NDC na kuazimia kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi wa chama ikiwa ni pamoja na kuwafukuza wanachama wa kundi pinzani.

 

NDC ilikuwa imeazimia kumfukuza aliyekuwa Mbunge wa Kieni Kanini Kega, ambaye amedai nafasi ya Katibu Mkuu, Mbunge mteule Sabina Chege na Mweka Hazina wa Kitaifa Nelson Dzuya.

 

Hata hivyo, kwenye barua iliyoandikwa Mei 29 na kuandikiwa Kioni, msajili wa vyama alifahamisha kambi ya Uhuru kwamba ombi la kuthibitisha mabadiliko hayo lilikataliwa kwa sababu ya kushindwa kuwasilisha stakabadhi kamili.

 

Msajili wa vyama Anne Nderitu alisema Kioni hakuwasilisha orodha iliyotiwa sahihi ya mahudhurio ya wajumbe katika NDC pamoja na nambari zao za vitambulisho ili afisi hiyo ibainishe muundo wa NDC na akidi.

 

Alisema hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 8.1[1] na 23 cha katiba ya chama cha Jubilee mtawalia.

 

Ofisi hiyo pia ilisema Kioni hakuwasilisha muhtasari wa kina wa NDC ili kubaini mchakato huo na utaratibu wa uchaguzi ikizingatiwa kuwa ni dondoo la dakika pekee ndilo lililowasilishwa.

 

Nderitu alisema Kioni alikuwa amewasilisha tu notisi ya kuitisha mkutano wa NDC wa Mei 22, 2023, notisi ya mabadiliko ya mahali na maazimio ya mkutano maalum wa NDC.

 

Wakati wa NDC, mrengo wa Uhuru ulimtaja Jamleck Kamau kama mkurugenzi wa kitaifa wa uchaguzi akidaiwa kuchukua nafasi ya Kega.

 

Chama pia kilimteua mwanablogu Pauline Njoroge kama naibu katibu mandalizi wake mpya huku Maison Leshomo akiwa mwenyekiti wa kitaifa wa ligi ya wanawake.

 

Mwanaharakati wa haki Maison Leshoomo aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kitaifa wa Ligi ya Wanawake huku Katibu Mkuu wa zamani Saitoti Torome akiteuliwa kuwa mwenyekiti wa kitaifa kuchukua nafasi ya Nelson Dzuiya.

 

Yasin Noor aliidhinishwa kama naibu katibu mkuu kuchukua nafasi ya Joshua Kutuny.

 

Katika mabadiliko hayo, chama kilikuwa kiwe na manaibu viongozi wanne wa chama. Wao ni Beatrice Gambo (mkakati), Maoka Maore (operesheni), Joseph Manje (programu) na Kados Muiruri (uhamasishaji).

 

Wengine waliofurushwa ni waliokuwa wabunge walioteuliwa Naomi Shaban, Boniface Kinoti, Jimi Angwenyi, Mutava Musyimi na Rachel Nyamai.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!