Mackenzie Kuzuiliwa Kwa Siku 60 Zaidi

Mchungaji Mackenzie Picha kwa hisani ya SIMON MAINA / AFP
Mchungaji Paul Mackenzie atazuiliwa kwa siku 60 ili kupisha uchunguzi ukamilike.
Katika ombi la kutaka kuongezewa muda, serikali inasema bado hawajahitimisha uchunguzi na wanahitaji muda zaidi.
Kulingana na mahakama Kurejeshwa rumande kwa muda ulioongezwa wa siku 60 ndicho kipindi kidogo zaidi kinachowezekana ambacho upelelezi unaweza kukamilika chini ya mazingira yaliyopo na ni njia zisizo na kikomo zaidi za kuhifadhi Uadilifu wa upelelezi nyeti.
Wanadai kuwa hakuna mabadiliko ya hali ya kuachiliwa huru kwa Mackenzie na washukiwa wengine 17 tangu uamuzi wa mahakama hiyo Mei 10 waliporudishwa rumande.
“Bado kuna sababu za msingi za kuwanyima dhamana hadi upelelezi ukamilike na kuna uwezekano mkubwa wa mashtaka makubwa dhidi ya washukiwa,” zinasoma hati za mahakama.