Daktari Mmoja Auawa Nanyuki

Polisi huko Nanyuki wanachunguza kifo cha daktari mmoja ambaye mwili wake ulipatikana nje ya ghorofa mapema hii leo Jumatano asubuhi.
Kulingana na Muchemi Wachira, chifu wa eneo hilo, alifahamishwa kuwa mwili uligunduliwa nje ya vyumba vya Serian Suites huko Nanyuki kati ya saa 4-5 asubuhi.
“Wakati tulifika hapa tukapata mwili unavunja damu, ndio tukaita polisi wakaja wakaanza uchunguzi,” Wachira alisema.
“Alikuwa amekatwa shingo na kudugwa na kisu kwa kifua,”
Mwili wa kiume unaonekana kuwa na majeraha shingoni na mgongoni kutokana na kitu chenye ncha kali, kulingana na uchunguzi wa awali.
Chifu wa eneo hilo alisema kuwa marehemu, John Mwangi, alikuwa mhudumu wa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Nanyuki lakini alikuwa amekubali kazi kwingine.
Maafisa wa Kituo cha Polisi cha Nanyuki wamesema kuwa marehemu alionekana kuuawa nyumbani kwake na mwili wake kutupwa nje ya ghorofa hiyo.
Msimamizi huyo alisema kuwa kulikuwa na njia ya damu kuelekea kwenye nyumba ya mwathiriwa, ambayo ilikuwa imefungwa, lakini funguo zilizolowa damu ziliachwa karibu.
“Tuliweza tukafungua ile nyumba pamoja na askari na kupata nyumba imelowa damu,’ chifu wa eneo hilo aliongeza.
“Hii Kitendo ilifanyika kwa nyumba halafu huu mwili ukaletwa hadi nje ya nyumba,”