Home » Bunge La Kenya Kufuata Nyayo Za Uganda

Licha ya ghadhabu ya kupitishwa kwa sheria ya kupinga ushoga nchini Uganda, Kenya inakabiliwa na hali sawa iwapo wabunge wataidhinisha mswada unaopiga marufuku ndoa za watu wa jinsia moja LGBTQ.

 

Wabunge wanaopaswa kurejelea vikao wiki ijayo, wanatarajiwa kushughulikia Mswada wa Ulinzi wa Familia 2023 unaofadhiliwa na Mbunge wa Homa Bay Mjini Peter Kaluma.

 

Mswada huo, ambao ulikuwa ukizingatiwa na Kamati ya Bajeti na Matumizi, unalenga kupiga marufuku ushoga, ndoa za jinsia moja, vitendo vya ngono visivyo vya asili na shughuli zinazohusiana Pia inalenga kuharamisha shughuli zinazolenga kukuza au kufadhili mapenzi ya jinsia moja.

 

Mswaada huo unataka wataobainika na makosa mbalimbali kujua adhabu ni kuanzia miaka kumi hadi kifungo cha maisha kwa watu binafsi kushiriki au kuendeleza ndoa za jinsia moja.

 

Mswada unaopendekezwa pia unalenga kubatilisha ndoa yoyote inayodaiwa au aina nyingine ya muungano ambayo ilifanyika kati ya watu au wapenzi wa jinsia moja.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!