Muungano Wa Maafisa Wa Kliniki Walalamikia Kucheleweshwa Kwa Mishahara
Muungano wa Maafisa wa Klinik nchini wameipa serikali muda wa siku 44 wa kufanya upya kandarasi kwa wahudumu elfu 9,000 wa huduma ya afya kwa wote UHC au wagome.
Maafisa hao wa kliniki pia wanadai malimbikizo ya mishahara wakisubiri kwa miezi mitatu.
Wakiongozwa na mwenyekiti wao Peterson Wachira, wahudumu hao wa afya pia wanataka Wizara ya Afya kuwajiri maafisa wa nyanjani kwa mafunzo yao.
Katibu Mkuu George Gibore kwa upande wake ametoa wito wa kutimizwa kwa makubaliano ya Rais Ruto Februari mwaka huu ambapo alisema kandarasi hizo zitaongezwa.
Maafisa wa chama hicho wametishia kuvamia makao makuu ya wizara katika Afya House siku ya Jumatatu iwapo wizara itashindwa kutimiza matakwa yao.
Aidha,0 ameongeza kwa kusema kwamba wamekuwa wakiwashirikisha kupitia mbinu ya kidiplomasia na kwa sasa wamesistiza kwamba kuanzia Jumatatu wiki ijayo, wataelekea kuomba barua zao za uteuzi katika Wizara ya Afya.