Home » Wanjigi :Ruto Anatupeleka Njia Ambayo Itafeli

Aliyekuwa Mgombea urais wa 2022 Jimi Wanjigi amemshtumu Rais William Ruto kwa kuchukua njia ambayo itasababisha uchumi wa nchi kuzorota.

 

Katika mahojiano na runinga, Wanjigi amesema Rais ameshindwa kusikiliza kilio cha umma katika mjadala kuhusu Mswada wa Fedha wa 2023, ambao umependekeza idadi kadhaa ya ushuru.

 

Kulingana na Wanjigi, serikali ya Ruto imeshindwa kuinua uchumi miezi minane baada ya kuchukua mamlaka na sasa inapanga kuwatoza Wakenya ushuru zaidi ili kutimiza majukumu yake ya kifedha.

 

Wanjigi anasema tangu kuchukua mamlaka, serikali ya sasa imeendelea kukopa pesa kutoka mataifa ya nje jambo ambalo limepelekea viwango vya deni la umma kupanda hadi viwango vya wasiwasi.

 

Wanjigi anasema ili serikali ifanikiwe, inabidi ipunguze kukopa na kushughulikia deni la sasa kwanza, kabla ya kufikiria deni zaidi.

 

Kulingana na data kutoka Benki Kuu ya Kenya, deni la umma la Kenya limevuka viwango vya udhibiti hadi Ksh. TRILIONI 9 SAWA NA (dola bilioni 72) kwa mara ya kwanza mnamo Desemba 2022.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!