Home » TSC Yaripoti Uhaba Wa Walimu

Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) imeomba kutengewa bajeti ya kila mwaka ya Ksh Bilioni.14.8 ili kukabiliana na uhaba wa walimu nchini.

 

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa TSC Nancy Macharia, alipokuwa akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya Uwiano ya Kitaifa ya Seneti amesema tume hiyo inahitaji walimu elfu mia 111,870 zaidi kwa muda wa miaka 5.

 

Tume imeweza kuajiri walimu elfu 30,000 pekee tangu Januari 2023.

 

Awali serikali ilikuwa imetangaza kuwa itaajiri walimu elfu 35,000 kufikia Septemba ili kuziba pengo hilo hasa katika shule za sekondari ya msingi ambako shughuli ya masomo imekuwa changamoto.

 

Macharia ameongeza kuwa tume hiyo itahitaji mgao wa bajeti wa kila mwaka wa Ksh BILIONI .14.8 kwa miaka mitano ijayo ili kupunguza tatizo hilo.

 

Wanakamati hata hivyo wamepinga pendekezo hilo wakisema huenda serikali isiweze kupata pesa zinazohitajika kuajiri walimu wa ziada.

 

Badala yake walipendekeza kuajiriwa kwa wafanyikazi ambao hatimaye wataajiriwa kwa masharti ya kudumu na ya pensheni.

 

Macharia hata hivyo amejibu kwa kusema kuwa TSC inawaajiri walimu waliohitimu zaidi akibainisha kuwa serikali ya Kenya Kwanza iliahidi kuajiri walimu elfu mia 116,000 itakapoingia madarakani.

 

TSC imefanikiwa kuajiri walimu elfu 36,000 katika zoezi lililoendeshwa Januari mwaka huu ambapo kati ya hizo nafasi elfu 30,550 zilitengewa shule za upili za chini, nafasi elfu 5,000 zikitengewa shule za msingi katika kaunti zote 47 na mia 450 zilipewa shule za upili.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!