Home » Rais Ruto Awakutanisha Viongozi Wa Afrika

Rais William Ruto amesisitiza umuhimu wa amani na usalama katika kuafikiwa kwa ajenda ya maendeleo ya Afrika.

 

Akiwahutubia wajumbe jijini Nairobi wakati wa ufunguzi wa kongamano la tatu la kimataifa la uwekezaji nchini Kenya, Ruto amesema ni jambo la kusikitisha kwamba eneo la Afrika linaendelea kukumbwa na migogoro ya mara kwa mara ambayo ambayo imedhoofisha juhudi zinazoendelea za kufanikisha uanzishwaji wa eneo la biashara huria la bara la Afrika.

 

Rais ruto ametoa wito kwa wabunge kuungana katika kuongeza uwezo wa pamoja na kufanikisha uwezo wake mkubwa kibiashara.

 

Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni miongoni mwa nchi za Kiafrika zinazokabiliwa na mizozo wenye madhara makubwa.

 

Mgogoro wa silaha kati ya makundi hasimu ya jeshi nchini Sudan ulioanza mwezi Aprili mwaka huu ambapo umeshuhudia vifo vingi na kusababisha karibu watu milioni 1.4 kuyahama makazi yao.

 

Mzozo unaoongezeka nchini DRC uliozuka mwaka wa 2022 wakati makundi yenye silaha yalipoanzisha mashambulizi mapya baada ya kukaa kwa miaka mingi na kusababisha zaidi ya watu milioni 20 kuhitaji msaada wa kibinadamu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!