Home » Mbunge Wa UDA Sylvanus Osoro Abadilisha Kauli

South Mugirango Sylvanus Osoro during a press conference in parliament on 8th.January.2020/EZEKIEL AMING'A


Kinara wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Sylvanus Osoro hii leo Jumatatu amebadilisha maoni yake kuhusu ushuru wa nyumba uliopendekezwa na Rais William Ruto.

 

Mbunge huyo wa Mugirango Kusini amekanusha kauli yake ya awali akisisitiza kuwa mswada huo utapitishwa na Bunge bila marekebisho yoyote.

 

Akizungumza kwenye runinga moja leo asubuhi, mbunge huyo amefichua kuwa Bunge la Kitaifa litafanya mabadiliko kwa mswada huo tata baada ya kukusanya maoni kutoka kwa washikadau.

 

Ameeleza kuwa ilikubaliwa baada ya kuzingatia kuwa mabadiliko yatafanywa kwa pendekezo hilo kwa kuzingatia maoni ya wananchi.

 

Kulingana na Osoro zaidi kwamba asilimia 3 ya ushuru wa nyumba za serikali na kodi mpya zilizomo katika Muswada huo ni pendekezo lililo wazi kwa ajili ya kuchunguzwa.

 

Mabadiliko ya Osoro yamejiri siku moja baada ya Rais William Ruto kuthibitisha kwamba utawala wake utaendelea na utekelezaji wa mpango wa nyumba za bei nafuu ambapo Wakenya wanaolipwa watakatwa asilimia 3 ya mapato yao ya kila mwezi.

 

Akizungumza wakati wa hafla ya kutoa shukrani katika Kaunti ya Busia, Ruto alieleza kuwa mswada huo unalenga kuziba pengo kati ya maskini na matajiri.

 

Matamshi yake yameungwa mkono na sekta ya Jua Kali na Muungano wa Wafanyabiashara wa Soko la Nairobi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!