Home » Polisi Wa Kupambana Na Ghasia Waweka Vizuizi Nakuru Kabla Ya Maina Njenga Kufikishwa Mahakamani

Polisi Wa Kupambana Na Ghasia Waweka Vizuizi Nakuru Kabla Ya Maina Njenga Kufikishwa Mahakamani

Polisi wa kupambana na ghasia mjini Nakuru wameweka vizuizi katika barabara zote zinazoelekea katika Mahakama ya Nakuru kabla ya kufikishwa mahakamani kwa aliyekuwa kiongozi wa Mungiki Maina Njenga.

 

Njenga anatazamiwa kukabiliwa na mashtaka kadhaa ya uhalifu miongoni mwao ya kuunga mkono kundi la uhalifu lililopigwa marufuku.

 

Njenga alikuwa amekashifiwa na maafisa wa upelelezi na makosa ya jinai DCI Alhamisi iliyopita jijini Nairobi kufuatia shutuma za kuhutubia mkutano eneo la Wanyororo kaunti ya Nakuru mnamo Mei 11, 2023 ili “kuhimiza uungwaji mkono” kwa kundi haramu la uhalifu, Mungiki.

 

Aidha anakabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na uhalifu. Anadaiwa kuwaalika watu binafsi kwenye mkutano huo eneo la Wanyororo ambako anadaiwa kutoa mwongozo unaohusiana na Mungiki.

 

Vile vile Anashutumiwa pia kwa kumiliki “kamba ya begi ya kijeshi, mali ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) ambayo inashukiwa kuibiwa au kupatikana isivyo halali.”

 

Kuonekana kwake katika makao makuu ya DCI hata hivyo kulikumbwa na vita baada ya maafisa wa polisi kutumia vitoa machozi kwa wafuasi wa Njenga ambao walikuwa wamejazana katika eneo hilo kumuunga mkono Njenga.

 

Pia anachunguzwa kuhusiana na kupatikana kwa bunduki mbili na zaidi ya misokoto 90 za bangi zilizopatikana katika nyumba inayohusishwa naye huko Ngomongo, Bahati.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!