Raila Kwa Ruto: Wasikilize Wakenya Au Ukabiliane Na Vita
Kiongozi wa muungano cha Azimio la Umoja One-Kenya Raila Odinga ameikashifu serikali ya Kenya Kwanza inayoongozwa na Rais William Ruto kwa madai ya kutotilia maanani masuala yanayoibuliwa na Wakenya kuhusu baadhi ya sera za utawala huo.
Odinga, katika taarifa yake kwa vyumba vya habari Jumamosi, aliitaka serikali kuanza kuwatilia maanani raia wa nchi, la sivyo itahatarisha kuanzisha uasi wa aina yake ambao haujawahi kushuhudiwa nchini Kenya.
Kulingana na kinara huyo wa upinzani, masuala ambayo upande wake umekuwa ukiibua na kupigania yana uhusiano zaidi na kuwalinda Wakenya kuliko kujinufaisha yeye mwenyewe.
Akitoa matakwa yake ya kufanyiwa mageuzi katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Odinga amesema kuwa bodi ya uchaguzi kama ilivyo sasa inaweza kusababisha machafuko nchini katika siku za usoni.
Waziri Mkuu huyo wa zamani aliunyooshea kidole utawala wa Rais Ruto kwa madai ya ukabila katika mchakato wake wa kuajiri, na hivyo kusema kuwa upinzani wake katika hili unalenga kusawazisha uwanja kwa Wakenya wengine walio na sifa sawa au zaidi ambao wanarukwa wakati wa ajira labda kwa sababu ya majina yao ya mwisho.
Aliendelea kueleza wasiwasi wake kuhusu ushuru wenye utata wa asilimia 3 ya mpango wa hazina ya nyumba, ambayo alisema wananchi wengi watashindwa kumudu kwa vile mfumo wao wa malipo tayari umejaa makato mengi ya kodi.
Pia alipuuzilia mbali pendekezo la kupandisha ushuru kwa bidhaa za urembo akisema litaumiza sekta hiyo ambayo ni tegemeo la mamilioni ya vijana.
Ikumbukwe kwamba raila ametishia kuanza mchakato wa kuwwashinikiza wakenya ili kugawa taifa kuwa sehemu mbili baada aya matakwa kukataliwa na kamati ya pande mbili hali iliyozua mgumzo miongoni mwa wakenya