Home » Duale Apuuzilia Mbali Mpango Wa Raila

Waziri wa Ulinzi Aden Duale amepuuzilia mbali mwito wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga wa kutaka kugawa taifa hili mara mbili baada ya matakwa yake kukatiliwa na kamati ya mazungumzo ya Kenya kwanza.

 

Waziri Duale amekashifu Odinga na kinara mwenza wa chama cha muungano cha Azimio la Umoja One Kenya Kalonzo Musyoka kuhusu maoni waliyotoa wakati wa mkutano huko Yatta, Kaunti ya Machakos, Ijumaa.

 

Viongozi wa Azimio walisema wangetoa wito wa kugawanywa kwa nchi katika sehemu mbili na itawalwe tofauti.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa manispaa ya Masalani katika Kaunti ya Garissa siku ya Jumamosi, Waziri Duale alitaja matamshi hayo kama mazungumzo ya kizembe na yasiyo na maana.

 

Ameendelea kutaja kuapishwa kwa Odinga kuwa Rais wa Wananchi’ baada ya uchaguzi wa 2017, akidai ni hatua nyingine ya kugawanya taifa.

 

Kulingana na Duale Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ameangukia kwenye mpango wa Odinga wakati wa kufanya mapinduzi wakati huu ambapo uchumi unaendelea kuzorota kutokana na serikali ya awali kuungana na Odinga ambaye alichangia kufeli kwa baadhi ya idara.

 

Waziri wa Ulinzi hata hivyo amemuonya Waziri Mkuu huyo wa zamani kuhusu athari mbaya ikiwa atafuata njia sawa na kujaribu kuyumbisha serikali ya Rais William Ruto.

 

Duale badala yake amemtaka kiongozi huyo wa upinzani kuheshimu Katiba, akibainisha kuwa utawala wa Kenya Kwanza hautatishwa na matakwa ya upinzani.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!