Home » Wanne Wajeruhiwa Katika Ajali Ya Basi La Easy Coach Sachangwan

Wanne Wajeruhiwa Katika Ajali Ya Basi La Easy Coach Sachangwan

Mojawapo ya basi ya Kampuni la Easy Coach/Picha kwa hisani

Watu wanne wamejeruhiwa hii leo Jumamosi asubuhi baada ya basi la Easy Coach kuhusika katika ajali kwenye barabara kuu ya Sachangwan huko Molo, Kaunti ya Nakuru.

 

Kampuni ya basi hilo katika taarifa, imesema watu waliojeruhiwa ni pamoja na abiria watatu na dereva.

 

Gari hilo lilikuwa likielekea Bondo Kaunti ya Siaya, kutoka Nairobi lilipohusika katika ajali hiyo mwendo wa saa tatu asubuhi.

 

Watu waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali ya Nakuru kwa matibabu huku abiria wengine wakiendelea na safari.

 

“Basi letu la Nairobi – Bondo 22.15 lilihusika katika ajali mwendo wa saa 9.00 asubuhi katika eneo la Sachangwany. Abiria watatu na dereva wetu walijeruhiwa na kupelekwa hospitali ya Nakuru kwa matibabu,” ilisema taarifa hiyo.

 

“Abiria wengine waliendelea na safari yao kuelekea Bondo kwa kutumia basi letu la Nakuru Rescue.”

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!